Tetesi zinasema, mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, anatazamia kuondoka Manchester United, huku Roma ya Jose Mourinho na Sporting Lisbon zikivutiwa naye.

Arsenal wana matumaini makubwa ya kumsajili fowadi wa Manchester City Mbrazil Gabriel Jesus, 25. The Gunners wanatumaini pauni milioni 30 zitatosha lakini City wanataka pauni milioni 50.

Lewandowski anayelengwa na Barcelona anasema bado anataka kuondoka Bayern lakini hataki kuharibu uhusiano wake na klabu hiyo ya Ujerumani kwa kulazimisha uhamisho.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema, Tottenham wapo mstari wa mbele kumsajili mlinzi wa Middlesbrough Muingereza Djed Spence, 21, huku Nottingham Forest wakihusishwa naye.

Manchester United wana imani Barcelona itapunguza bei yao ya pauni milioni 73 ili kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, kwa sababu ya matatizo yao ya kifedha.

Tetesi zinasema, West Ham wako tayari kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wa Croatia Nikola Vlasic, 24, huku Hadjuk Split na Torino wakimtaka.

Tetesi zinasema, Sevilla wako tayari kutoa £6.9m kwa mshambuliaji wa Rangers na Colombia Alfredo Morelos, 25.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema, Fulham wako tayari kukamilisha usajili wa pauni milioni 7 wa mshambuliaji wa Israel Manor Solomon, 22, kutoka Shakhtar Donetsk.

Mshambuliaji wa Watford wa Nigeria Emmanuel Dennis, 24, yuko kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa na Everton msimu huu ikiwa mshambuliaji wao wa Brazil Richarlison, 25, ataondoka.

Paris St-Germain wanatazamiwa kuzishinda timu kadhaa za Premier League hadi kufikia pauni milioni 34 kumsajili kiungo wa kati wa Porto Mreno Vitinha, 22.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa