Tetesi zinasema, Klabu ya Inter Milan ya Italia imekubali dili la kumsajili mshambuliaji Romelu Lukaku kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Chelsea.

Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski bado anataka kuondoka Bayern Munich, licha ya mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Ujerumani Hasan Salihamidzic kusafiri kukutana na mchezaji huyo na kujaribu kubadilisha mawazo yake.

Tetesi zinasema, Real Madrid wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumnunua mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling anaewindwa na Chelsea katika wiki za hivi karibuni.


 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema, Real Madrid, Bayern Munich na Paris St-Germain wako tayari kuchuana na Newcastle United kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Hugo Ekitike, 20, kutoka Reims.

Barcelona wanataka kumsajili beki wa Ufaransa Jules Kounde, lakini hawataki kulipa euro milioni 60 za Sevilla (£51.5m) kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.

Brentford haijakata tamaa ya kumsajili mchezaji wa Denmark Christian Eriksen, ambaye alijiunga nao kwa mkopo mwezi Januari kabla ya kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita. Manchester United pia wanavutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.

Tetesi zinasema, Arsenal na Newcastle wanamtaka kiungo wa kati wa Uhispania Fabian Ruiz, 26, ambaye mkataba wake na Napoli utakamilika 2023.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema, Chelsea wanavutiwa na beki wa pembeni wa Lens, 29, Jonathan Clauss.

Wolves wanatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Brazil Gabriel Barbosa, 25, kutoka Flamengo na kiungo wa kati wa Argentina Enzo Fernandez, 21, kutoka River Plate.

Rangers wanaweza kumuuza mshambuliaji wa Colombia Alfredo Morelos ikiwa hawatakubaliana mkataba mpya na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika msimu wa joto 2023.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa