Tetesi zinasema winga mshambuliaji wa Ajax na Brazil, Antony, 22, amedhamiria kujiunga na Manchester United msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema, beki wa pembeni wa Manchester United Muingereza Brandon Williams, 21, anaweza kuuzwa kwa £10m.

Ajax wanatazamiwa kuwasilisha ofa nyingine kwa winga wa Tottenham Hotspur na Uholanzi Steven Bergwijn, 24, lakini klabu hiyo ya Premier League haitakubali ofa ya chini ya pauni milioni 25.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Southampton wamejaribu kuzuia nia ya Manchester City, Manchester United, Tottenham na West Ham kumnunua kiungo wa kati wa England James Ward-Prowse, 27, kwa dau la pauni milioni 75.

Afisa mtendaji wa Bayern Munich Oliver Kahn anasema anatarajia fowadi wa Poland Robert Lewandowski, 33, kusalia na mabingwa hao wa Ujerumani msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema, Manchester City wapo kwenye mazungumzo ya juu zaidi ya kutaka kumsajili beki wa Brighton na Uhispania Marc Cucurella, 23.

Meneja wa Barcelona, Xavi anamsihi winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 25, kusaini kandarasi mpya huku Chelsea ikimuwinda winga huyo.

 

Dembele

Tetesi zinasema, Nice wanataka kumsajili kwa mkopo mlinda lango wa Chelsea Mhispania Kepa Arrizabalaga, 27.

Mshambulizi wa Chelsea na Albania Armando Broja, 20, atakuwa tayari kujiunga na West Ham endapo klabu hiyo itawasilisha dau la pauni milioni 25.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Real Madrid na Uhispania Marco Asensio, 26, anatamani kujiunga na Liverpool badala ya AC Milan.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa