Tetesi zinasema, mshambuliaji wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo, 37, ilikuwa mojawapo ya mada zilizojadiliwa wakati mmiliki mpya wa Chelsea Todd Boehly alipokutana na wakala wa mchezaji huyo Jorge Mendes wiki iliyopita.

Tetesi zinasema, Chelsea huenda wakamuongeza mshambuliaji wao wa Ujerumani Timo Werner, 26, katika mkataba wa kubadilishana mlinzi wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, 22.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema, Ronaldo anaweza kurejea Ureno baada ya klabu yake ya kwanza ya Sporting Lisbon kumpigia debe kuhusu kurejea nyumbani.

Manchester United wanazidi kuwa na uhakika wa kumpata mchezaji Frenkie de Jong, huku ada ya maafikiano ya takriban £69m kufikiwa na Barcelona kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi, 25.

Porto wanatarajia Liverpool kuimarisha nia yao ya kumnunua winga wa Ureno Otavio, 27, wiki hii baada ya kukataa ofa ya pauni milioni 26 kutoka Leeds United.

Arsenal wanatazamiwa kuongeza juhudi zao za kumsajili mshambuliaji wa Leeds na Brazil Raphinha, huku klabu hiyo ya London ikifikiriwa kuwa inapewa nafasi kubwa ya kufunga mkataba wa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.

Tetesi zinasema, Juventus na Paris St-Germain wameanzisha mazungumzo yanayohusu kumnunua mshambuliaji wa Brazil Neymar, 30, ambaye pia anahusishwa na Chelsea.

Neymar

Mkufunzi wa Chelsea Thomas Tuchel amewasiliana na mshambuliaji wa Manchester City na Muingereza Raheem Sterling, 27, huku kukiwa na nia ya klabu hiyo ya London.

Tetesi zinasema, Everton na Tottenham wanaendelea na mazungumzo yao kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati wa Spurs na Uingereza Harry Winks, 26.

Winga wa Uingereza Malcolm Ebiowei, 18, alikataa nafasi ya kujiunga na Manchester United akipendelea kuhamia Crystal Palace kwa uhamisho wa bure kutoka Derby.

Beki Samuel Umtiti, 28, ataondoka Barcelona msimu huu wa joto, huku Girona na timu nyingine kadhaa za Serie A zikimhitaji mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.

Tetesi zinasema, mshambuliaji wa Real Madrid na Uhispania Marco Asensio, 26, na kiungo wa kati Dani Ceballos, 25, wanatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa