Tetesi zinasema, Arsenal wana uhakika wa kuipiku Manchester United kwenye usajili wa pauni milioni 30 wa kiungo wa kati wa Leicester na Ubelgiji Youri Tielemans, 25.

Manchester United wametoa dau la pauni milioni 51 kumnunua mshambuliaji wa Ajax Mbrazil Antony, 22, lakini klabu hiyo ya Uholanzi inashikilia dau la £68m.

Tetesi zinasema, Chelsea inaandaa dau la pauni milioni 38 kumnunua kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Matheus Nunes, ambaye pia analengwa na Wolves.

 

tetesi, Tetesi za soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema, Everton wanajiandaa kumpa winga wa England chini ya umri wa miaka 21 Anthony Gordon, 21, mkataba mpya ili kuzuia nia ya Newcastle.

Leeds wamewataka Barcelona kutoa ofa ya mwisho kwa Raphinha wiki hii kwani wanataka mustakabali wa mshambuliaji huyo wa Brazili kutatuliwa haraka iwezekanavyo.

Crystal Palace wana matumaini ya kuzishinda Everton na Nottingham Forest katika kumnasa kiungo wa kati wa Wolves Muingereza Morgan Gibbs-White, 22.

Tetesi zinasema, Crystal Palace wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Swansea Muingereza Flynn Downes, 23, kwa £8m.

 

Pepe

Arsenal wanataka kuuza wachezaji saba – akiwemo winga wa Ivory Coast na aliyesajiliwa kwa rekodi ya klabu Nicolas Pepe, 27, na mlinda mlango wa Ujerumani Bernd Leno – ili kufadhili matumizi ya wachezaji wengine wapya.

Tetesi zinasema, Tottenham wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 15 wa beki wa pembeni wa England chini ya miaka 21 Djed Spence kutoka Middlesbrough.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa