Tetesi zinasema, Chelsea wanaweza kuwatoa Cesar Azpilicueta, 32, na Marcos Alonso, 31, pamoja na pauni milioni 51 ili kuwapiku Manchester United katika mbio za kumsajili kiungo wa Barcelona, Frenkie de Jong, 25.

Manchester United wako tayari kusikiliza ofa kwa Cristiano Ronaldo msimu huu wa joto huku Chelsea na Napoli wakimtaka mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 37.

Tetesi zinasema, Tottenham wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa kati wa Barcelona na Ufaransa Clement Lenglet, 27, kwa mkataba wa mkopo wa msimu mzima.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Manchester United wametakiwa kulipa ada ya uhamisho ya pauni milioni 106 ili kuwasajili mlinzi wa Argentina Lisandro Martinez, 24, na winga wa Brazil Antony, 22, kutoka Ajax.

Mkufunzi wa Brentford Thomas Frank anasisitiza kuwa klabu ya London Magharibi haikati tamaa katika kumsajili kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 30, ambaye anatarajiwa kujiunga na Manchester United.

Tetesi zinasema, Arsenal wanafikiria kumnunua beki wa kushoto wa Benfica Mhispania Alex Grimaldo, 26, huku Mikel Arteta akitamani kuongeza ulinzi kwa Kieran Tierney.

Chelsea wanatazamia kumpa beki wa pembeni wa England Reece James, 22, nyongeza ya kandarasi, licha ya mkataba wake wa sasa kukamilika Juni 2025, ili kuzuia nia ya Manchester City na Real Madrid.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet
Reece James

Chelsea bado wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili Raphinha, 25 kwa pauni milioni 55, huku Leeds bado wakisubiri ofa kutoka kwa Barcelona kwaajili ya mshambuliaji huyo wa Brazil.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji Fabio Silva, 19, anatazamiwa kujiunga na Anderlecht kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Wolves, ambao walimnunua kwa £35m miaka miwili iliyopita.

Tetesi zinasema, Leeds wako tayari kulipa kiasi cha kuvunja rekodi ya klabu cha £31.6m kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Charles de Ketelaere kutoka Club Bruges, 21.

Tetesi zinasema, Newcastle bado wako kwenye mazungumzo na Everton kuhusu uwezekano wa kumnunua winga Mwingereza Anthony Gordon, 21.

Bashiri sasa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa