Tetesi za Soka Barani Ulaya.


Tetesi zinaasema Manchester United wiki ijayo itaweka mezani dau la mwisho la £90m kwa ajili ya kujaribu kumsajili winga wa England Jadon Sancho, 20, kutoka Borussia Dortmund.

Tetesi zinasema Arsenal wameonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Chelsea na Italia Jorginho, 28.

Lucas Torreira anakaribia kuondoka Arsenal, huku klabu za Atletico Madrid na Torino zikionyesha nia ya kumnasa kiungo huyo wa Uruguay, 24.

Atletico Madrid wanaamini watamnasa Torreira kwa mkopo, hatua itakayoifanya Arsenal nayo kumsajili kiungo wa timu hiyo ya Hispania Thomas Partey, 27, raia wa Ghana.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.
 

Manchester City imesema madai kwamba imeweka ofa ya £78m kwa ajili ya mlinzi wa Atletico Madrid na Uruguay Jose Gimenez, 25, sio kweli.

Tetesi zinasema Monaco imeonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Tottenham na England Dele Alli, 24,

Paris St-Germain wanatarajia kujiondoa kwenye mazungumzo ya kumsajili Alli kwa mkopo wa muda mrefu.

Mshambuliaji wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi, 19, anataka kuondoka Stamford Bridge kwa mkopo .

Kiungo mchezeshaji wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho, 28, anaweza kwenda kwa mkopo Arsenal kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

RB Leipzig wanakaribia kumsajili mlinzi wa kati, hatua itakayosaidia mlinzi wake Dayot Upamecano kuondoka klabuni hapo. Manchester United imekuwa ikihusishwa kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21.

Mshambuliaji wa Napoli Arkadiusz Milik amewekwa sokoni kwa kikosi cha Everton cha Meneja Carlo Ancelotti, lakini Muitaliano huyo akiwa na joto la kutaka kuungana nae tena nyota huyo wa kimataifa wa Poland, 26.

Sheffield United inaongoza mbio za kumsajili mshambuliaji wa Liverpool , Muingereza Rhian Brewster, 20, huku klabu za Aston Villa, Brighton na Crystal Palace zikionyesha nia ya kumsajili.

West Ham na Aston Villa ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka kumsajili kiungo wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek, 24, kwa mkopo wa msimu mzima.

Southampton wanatarajia pia kukamilisha usajili wa kiungo wa Toulouse na Ivory Coast Ibrahim Sangare, 22.

Tetesi zinasema Everton na Fulham wanamuania mlinzi wa Cameroon Jerome Onguene, 23, kutoka RB Salzburg.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

West Brom wanaweza kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester City Emmanuel Adebayor, 36, kama watashindwa kumnasa mshambuliaji mwingine kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Mlinzi wa St Etienne Wesley Fofana anaweza kutua Leicester City lakini mpango wowote utakaokubaliwa utakaomfanya kinda huyo wa umri wa miaka 19 asalie kwenye Klabu hiyo ya Ufaransa.

Tetesi zinasema Meneja wa Southampton Ralph Hasenhuttl anataka kusajili wachezaji watatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Bayern Munich hawatamruhusu kiungo wa Ufaransa Michael Cuisance kuondoka kwa mkopo, licha ya Leeds United na Marseille kuripotiwa kuonyesha nia ya kumsajili nyota huyo wa umri wa miaka 21.


FURAHIA KASINO YA MTANDAONI

Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.

Cheza Sasa

29 Komentara

    united hawataki kukata tamaa kabisa juu ya kumsajili sancho

    Jibu

    Manchester united wafanye juhudi ili waweze kumchukuwa Sancho

    Jibu

    Arsenal wameonyesha nia ya kumsajili Jorginho imekaa poa sana kuelekea kukiandaa kikosi kuwa kizur zaid

    Jibu

    Gud

    Jibu

    United naona bado wanampambania sancho hawataki kabisa kukata tamaa juu ya kumsajili

    Jibu

    Koeman kashasema coutinho yupo kwenye mipango yake

    Jibu

    Man Chester united wanapigania sana sain ya sancho

    Jibu

    Man U fanyeni mpango mchukue jembe hilo.

    Jibu

    Safi sana man

    Jibu

    Man U haijakata tamaa kumutaka Jadon Sancho#meridianbettz

    Jibu

    Inabidi ifike mahali wakubaliane

    Jibu

    Man u inabidi wasikate tamaa kwenye usajili wa sancho lazima aje man u

    Jibu

    Nice 👍

    Jibu

    Man U fanyeni mpango kiereweke

    Jibu

    Safi sana man

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Usajili umepamba moto kila mtu anajiandaa ipasavyo

    Jibu

    Good

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Ongezeni dau mambo yasiwe mengi,kizuri gharama!!!

    Jibu

    United waache maneno wamchukue sancho

    Jibu

    Zko vzur sana

    Jibu

    Gud news 👍

    Jibu

    Man utd kazeni buti mumpate sancho

    Jibu

    Man u wamchukue sancho wasilet maneno

    Jibu

    Man u hawakati tamaa

    Jibu

    ahsante kwa taarifa

    Jibu

    Duh ili Dau la Sancho pasua kichwa

    Jibu

    Arsenal wameonyesha nia ya kumsajili Jorginho imekaa poa sana kuelekea kukiandaa kikosi kuwa kizur zaid

    Jibu

Acha ujumbe