Tetesi zinasema Manchester United imejiondoa katika kumsaini mshambuliaji wa England Jadon Sancho 20, baada ya kubaini kwamba uhamisho huo huenda ukaigharimu timu hiyo £227m kutokana na dau la £108m linalotakiwa na Borussia Dortmund , pamoja na mahitaji ya marupurupu ya mshahara kutoka kwa ajenti wake.
West Ham walikuwa wako tayari kumsaini beki wa England Fikayo Tomori, 22, kwa mkopo ambao walikuwa wamejitolea kuilipa Chelsea dau la £50,000 kila mara alipokosa kuwachezea The Hammers , lakini makubaliano hayo hayakuafikiwa.

Tetesi zinasema Tottenham na West Ham wana hamu ya beki wa kati wa Wales Joe Rodon, 22, na huenda wakawasilisha ombi la dau la £18m kabla ya siku ya mwisho ya ligi ya EFL mnamo tarehe 16.
Tetesi zinasema West Ham huenda ikawasilisha ombi la kumsajili beki wa Watford na England Craig Dawson, 30, lakini watahitajika kulipa £4m.
Ombi la Manchester United la kumsajili winga wa Senegal Ismaila Sarr kwa kipindi kilichosalia cha msimu huu lilikataliwa na Watford , lakini inaweza kujaribu tena mwezi huu licha ya kwamba The hornets wanataka mkataba wa kudumu.

Kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum amepuuzilia kujiunga na klabu ya Barcelona. Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 inakamilika msimu ujao Anfield.
Klabu ya Ufaransa ya Saint-Etienne imeikosoa Arsenal kwa kushindwa kumruhusu beki kinda wa Ufaransa William Saliba kurudi katika klabu hiyo.
Barcelona itasubiri hadi mwisho wa msimu wa 2021 ili kumsajili beki wa Uhispania Eric Garcia, 19, kutoka Manchester City. Barca ilitoa Euro milioni 2 katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho.

Jaribio la Barcelona kumsaini mshambuliaji wa Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 26, lilishindikana baada ya winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 23, kukataa kujiunga na Manchester United.
Tetesi zinasema Watford na Middlesbrough inamtaka beki wa kushoto wa Chelsea na Ghana baba Rahman , 26, kwa mkopo wa muda mrefu.
Sasa unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwenye akunti yako ya Meridianbet kwa kutumia mtandao wa Airtel. Usipate wasi wasi, tunaifanya kazi kuwa rahisi zaidi!



Mwajumah
Man united mmefanya makosa sana kumuacha sancho kwan angeleta matokeo mazuri kwenye clabu
Amani
Man u wamefanya usajili wa ovyo kabisa
Zeiyana
Man wapambanie saini ya sancho hatawafaa sana
magdalena
afadhali kama united wamejitoa katika kumchukua sancho
Dorophina
Nilijua tu man u hana uwezo wa kumnunua sancho
Angelina
Goodupdate
Adelta
Man u wamchukuwe kwa sababu Sancho Yuko vizuri na anajuwa vyema anachokifanya
Fatina mfingi
Daah inabid wapambane ili wapate sain yake sanch
Sauda
Man U wanatakiwa kujipanga kwenye usajili
Elika
Man u watulie akili kidigo
Rose kapinga
Pesa ndio kila kitu!!!
Johnmary jo
Hapo watafute pesa yakutosha watampata kwasababu vitu vizuri lazima uvigalimie#meridianbett
Shafii
Zimekaa poa
Caroline
Asante kwa taarifa
farida ahmadi
Manchester United sijui wanakwama wapi
Amiri Kayera
Sancho wangepgw t pesa nying watulie
Salma ngende
Iko vizuri
latifa juma mohamed
Zimekaa poa tu.
Samiah
Ipo vzr
Nasra
Asantee kwa taarifa
Fatuma kasomo
Gud news
Shani
Man United imekua tatizo kwa usajili w sancho
David Pere
West Ham walikuwa wako tayari kumsaini beki wa England Fikayo Tomori, 22, kwa mkopo ambao walikuwa wamejitolea kuilipa Chelsea dau la £50,000 kila mara alipokosa kuwachezea The Hammers , lakini makubaliano hayo hayakuafikiwa.
Hidaya
Man u wazinguaji tu
Saupha mohamed
Man u ni shida sana
Hopemwaikuka
Imeeleweka sana
Neema
Imekaa bomba
aisha
Mambo ya sokoa hayo
Samira
Sancho angetua utd mambo yangebadilika
Issa
United imefeli katika dirisha hili hamn usajil huyo cavan kama umri umesonga
Povel
Usajil ni moto Epl
Sabrina
Man u majanga tu wamesajili utopolo
felister
ahsante kwa taarifa
Rehema
Mambo ni moto
Tatu
Bora man u walivyotuka mapema ugaili kumsajili sancho bila hvyo wangefilisika wajalibu tu kungine
Theckla
Taarifa nzuri
Lydia Emmanuel Magoti
Nawashangaa Sana Man U kwanini Sain ya Sancho bado inawagalagaza
Gabriel
Imekaa poa Sana
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif