Tetesi za Soka Barani Ulaya.


Tetesi zinasema Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amesema kuwa amempatia mchezaji nyota wa zamani wa klabu hiyo Mesut Ozil ,32, “nafasi nyingi” kadri ya uwezo wake kabla ya kumuacha nje ya kikosi cha Ligi ya Primia na Ligi ya Europa.

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola, ambaye kandarasi yake katika klabu hiyo inamalizika msimu ujao amepuuzilia mbali tetesi zinazomhusisha na kurejea Barcelona.

Tetesi zinasema Barcelona inatarajiwa kurejelea tena jitihada za kumsajili mlinzi wa miaka 19 wa Manchester City Eric Garcia mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguliwa.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Carlo Ancelotti anasisitiza kuwa mshambuliaji Moise Kean,20 atarejea msimu ujao kujiunga na Everton mkataba wake wa mkopo Paris St-Germain utakapokamilika.

Mkufunzi wa Bayern Munich Hansi Flick ana matumaini kuwa mlinzi wake David Alaba, 28, raia wa Austria atakubali kutia saini kandarasi mpya ya kusalia katika klabu hiyo.

Kocha wa England Gareth Southgate anajiandaa kumjumuisha beki wa kulia na nyuma wa Manchester Luke Shaw, 25, katika kikosi cha kimataifa, baada ya kumteua tangu mwezi Machi mwaka 2019.

Nyota wa Wales na Spurs Gareth Bale ametoa msaada wa £15,000 kufadhili zawadi 300 za Krismasi zitakazopewa watoto walio na uhitaji zaidi Wales.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema Mkurugenzi wa soka wa Arsenal Huss Fahmy anatarajiwa kuondoka klabu baada ya kujiunga na Gunners miaka mitatiu iliyopita.

Wakala wa ngazi ya juu Mino Raiola amewasili AC Milan kuanza mazungumzo ya kurefusha mkataba wa kipa Gianluigi Donnarumma, 21, na mlinzi Alessio Romagnoli, 25.

Tetesi zinasema Atletico Madrid wanajiandaa kumsajili kiungo wa kati wa Valencia na Jamhuri ya Afrika ya Kati Geoffrey Kondogbia, 27.

Derby County inakaribia kununuliwa na Sheikh Khaled bin Zayed Al Nehayan of Abu Dhabi, ndugu wa mmiliki wa Manchester City Sheikh Mansour.


TSH.160,000,000 KUSHINDANIWA!

Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.

Kamata Mkwanja wako HAPA

24 Komentara

    Ziko vizuri na zinasomeka

    Jibu

    Sasa matunda mema kwa bale yanaonekana hongera sana

    Jibu

    Barcelona wakimpata Eric Garcia watakuwa wamelamba dume.

    Jibu

    Hongerin arsenal kwa kupata jembe!

    Jibu

    Bale katisha

    Jibu

    ongera sana bale

    Jibu

    Bale yupo vzr

    Jibu

    Good job bale

    Jibu

    Safii Sana bale

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Bale yuko fiti

    Jibu

    Hongera sana Bale

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Bale Yuko vizurii

    Jibu

    Barcelona wameamua kuongeza wachezaji

    Jibu

    Sio mbaya

    Jibu

    safi sana

    Jibu

    Ozil tafuta chaka

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Bale yuko vizuri sana

    Jibu

    Ozil yupo vizuri

    Jibu

    Habari poa sana

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

Acha ujumbe