Tetesi za Usajili

Straika wa Everton Moise Kean, 20, amehusishwa kujiunga na Napoli. Kean anaweza kuchukuliwa hatua za nidhamu na Everton baada ya kuvunja sheria serikali kuhusu Virusi vya Corona mapema wiki hii.

Arsenal wametuma ofa kwa winga wa Chelsea, Willian, 31, Mbrazili huyo atakuwa mbadala wa straika wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang laini washika mitutu wameshtushwa na mshahara anaotaka.

Arsenal wamepeleka ofa ya £43m kwa Atletico Madrid ili kumnasa kiungo Mghana Thomas Partey, 26.

Barcelona wamefanya kiungo wao wa Brazili Philippe Coutinho, 27, mshambuliaji wake wa Ufaransa Ousmane Dembele, 22, kuwepo kwaajili ya mabadilishano kipindi cha kiangazi.

Chelsea wameachana na nia ya kumsajili Coutinho sasa wanamuwinda kiungo wa Bayer Leverkusen na  Ujerumani Kai Havertz, 20.

West Ham United wanaweza kulazimika kumuuza kiungo wa Uingereza Declan Rice ili kusaidia klabu kiuchumi, Chelsea na Manchester United wanamuwania.

Liverpool wapo katika nafasi nzuri ya kumsaini straika wa Lille, Victor Osimhen, 21, japo watapata upinzani kutoka kwa Leicester na Chelsea.

Mkurugenzi wa Michezo Borussia Dortmund “tumepumzika kabisa” kuhusu hatma Jadon Sancho. Winga huyo wa Uingereza amkuwa akihusishwa kujiunga na Manchester United.

Sancho

Japo, United wanatakiwa kuuza viungo wawili, Mfaransa Paul Pogba na Muingereza Jesse Lingard, ili kutafuta pesa ya kumsajili Sancho.

Manchester United wamehusishwa kumsajili beki wa Real Valladolid Mohammed Salisu, 21.

Kiungo wa Leicester City, Wilfred Ndidi amesema anafurahia maisha klabuni, pamoja na kiungo huyo kuwaniwa na Manchester United na Arsenal.

Kiungo Dani Ceballos, 23, amesema ana matumaini ya kurejea Real Madrid baada ya kumaliza dili la mkopo wa msimu mzima akiwa Arsenal.

Kocha wa zamani wa Spurs na Chelsea, Andre Villas-Boas amesema hatarejea tena EPL.

2 Komentara

    corona sio ugonjwa wa mchezo

    Jibu

    Asante kwa taarifa meridianbettz

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.