Tetesi za Usajili

Klabu ya Juventus inaamini kwamba bado matumaini yao ya kumuondoa nyota wao Dyabala kujiunga na klabu nyingine litaweza kufanikiwa kutokana na uhitaji wao kutaka kupunguza matumizi ndani ya klabu yao na kutaka kuweka vitabu vyao sawa ili kuzuia kukutana na adhabu za Shirikisho la Soka Duniani.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya PSG, Leonardo amesema kwamba nyota wa klabu hiyo na raia wa Brazil, Neymar amefanya makosa makubwa sana. Amesisitiza kwamba nyota huyo bado ana mkataba na klabu yao wa miaka miwili kwa hiyo jambo hilo haliwatishi hata kelele zikipigwa na klabu nyingine.

Mbali na Eriksen kusema kwamba hatamani kuendelea kucheza soka lake nchini Uingereza kama akitokea kuondoka Tottenham lakini kocha wa klabu ya Manchester United anataka kumshawishi kiungo huyo ili aweze kujiunga na klabu yao. Ole anatamani sana kufanya kazi na nyota huyo mwenye kipaji cha pekee sana uwanjani.

Baada ya kuvuma sana kwa taarifa kwamba Manchester United walikuwa na nia ya pekee kabisa kutaka kumsajili nyota wa klabu hiyo na raia wa Senegal, Koulibaly basi taarifa za ndani ya klabu hiyo zinadai kwamba Napoli waligomea dili hilo la £82m ili kumuuza nyota huyo. Usajili huo ungefanikiwa ulikuwa ni wenye kuvunja historia kwa dau hilo kwa mlinzi kutoka Afrika.

Nyota na raia wa Brazil aliyekuwa akikipiga na Barcelona, Coutinho kwa sasa amefanikiwa kujiunga na klabu ya Bayern Munich baada ya kufikia makubaliano na klabu yake hiyo na kuwa na kipindi kirefu cha fununu kwamba angeweza kutimka klabuni hapo. Kwa sasa nyota huyo atakuwa na mfungaji wa muda wote wa ligi hiyo, Lewandowski wakikipa nguvu kikosi cha timu hiyo.

Mlinzi wa klabu ya Manchester United na raia wa Uingereza, Maguire amekiri kwamba aligomea ofa ya kujiunga na mahasimu wake, City pamoja na kutengewa dau nono iwapo angejiunga nao. Kwake yeye alichokuwa anakiangalia klabuni hapo ni nafasi ya kuonesha ufundi wake uwanjani na ndiyo maana aliona kwa hilo United ni chaguo lake.

Acha ujumbe