Tetesi za Usajili Bongo

Nyota wa Klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe, Perfect Chikwende yupo kwenye hesabu za mabosi wa Klabu ya Azam FC.

Jina la Chikwende kiungo wa FC Platinum ghafla limekuwa maarufu ndani ya ardhi ya Bongo baada ya kuwatungua Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa.

Desemba 23, Simba ikiwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 1-0 na mtibuaji mipango akiwa ni nyota huyo dakika ya 17.

Ousmane Adama Ouattara beki kitasa wa Klabu ya AS Vita ya Congo anatajwa kuingia kwenye rada za mabosi wa Yanga.

Licha ya Yanga kutokuwa na shida kwenye nafasi ya ulinzi kwa sasa habari zinaeleza kuwa mpango mkubwa wa kikosi hicho ni kuwa na wachezaji matata hata wale watakaokaa benchi.

Ikiwa inaongoza Ligi Kuu Bara na pointi 43 imefungwa mabao sita kati ya mechi 17 kwa msimu wa 2020/21 na safu yao ya ulinzi inaongozwa na nahodha Lamine Mono raia wa Ghana.

Mshambuliaji wa APR ya Rwanda Jacques Tuyisenge, ambaye amekuwa akitajwa kuibukia ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa kwa sasa haruhusiwi kuzungumza na timu yoyote kwa kuwa ana mkataba na tmu aliyopo.

Tuyisenge mwenye uraia wa Rwanda, aliwahi kutamba katika kikosi cha Gor Mahia akiwa sambamba na nyota wa sasa wa Simba, Meddie Kagere, Francis Kahata na Joash Onyango.

Kocha wa AS Vita ya DR Congo, Florent Ibenge ambaye alihusika kwenye dili za wachezaji Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe kutua Yanga, anatajwa kuwa yuko mbioni kulishusha jembe jipya ndani ya kikosi hicho.

Jembe jipya ambalo linaletwa na Ibenge ni straika Dark Kadima Kabangu anayeitumikia DC Motema Pembe ya nchini humo.

 


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

12 Komentara

    Usajili umepamba moto

    Jibu

    Mhh usajili atari

    Jibu

    Usajili umekuwa moto asaiv

    Jibu

    Mambo ya usajili hayo

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Usajili bongo unazidi kunoga

    Jibu

    Tuyisenge njoo yanga

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Bongo Mambo ni hoya hoya

    Jibu

    Sawaa nmeelewa

    Jibu

    Naona azam wanaanza kujilipua

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.