Tetesi za Usajili Ulaya

Baada ya kuachana na Spurs sasa kilichosalia ni klabu hiyo kulipa fidia kwa kocha huyo itakayotokana na kumvunjia mkataba. Kwa mujibu wa utaratibu pale klabu inapovunja kandarasi ya mtu hupaswa kulipa fidia inayostahili. Fidia atakayolipwa kocha hiyo inalingana na ile ambayo United waliilipa kwa Mourinho pindi wanamtimua kikosini hapo.

Klabu ya Manchester City imeanza mazungumzo ya karibu na mchezaji wao raia wa Uingereza, Raheem Sterling juu ya kumuongezea mkataba kusalia kikosini hapo. Nyota huyo yupo kwenye kiwango ambacho kwa namna yoyote ile City watamshawishi  atulie na kikosi chao.

Inasemekana kati ya vitu vilivyomuondoa Pochettino klabuni ni zoezi zima la kulumbana na wachezaji wake katika vyumba vya kubadilishia nguo kutokana na matokeo mabovu. Baadaye uongozi chini ya Levy ukamtaka kocha huyo ajiondoe lakini kocha huyo aligomea maamuzi hayo ndipo ikapelekea kutimuliwa na matajiri wake hao.

Manchester United ipo mawindoni kwa sasa ikiangalia kwa jicho la pekee wachezaji watakaobeba taswira ya kikosi chao. Kwa sasa wapo mbioni kumuangalia nyota wa Norway ambaye atatumia mgongo wa kuaminiwa na Ole, Haaland anayekadiriwa kuwa na gharama ya hadi £85m kama United wataamua kuvunja kibubu.

Nahodha wa zamani wa Chelsea, John Terry ametupilia mbali uvumi unaodai kwamba alikuwa ni sehemu ya watu walioshawishi kutosajiliwa kwa Aguero katika kikosi cha Chelsea kipindi cha nyuma kabla ya nyota huyo kutambulika na kusajiliwa na Manchester City.

Wachezaji wa Manchester United wameonywa kutokana na hali ya hewa kwenye mechi yao ya Europa itakayopigwa huko Kazakhstan. Wamepata onyo la kutokutoka nje kwa zaidi ya dakika kumi. United watacheza mechi ya ligi hiyo dhidi ya FC Astana ikiwa ni hatua ya kundi lao kufuzu kusonga hatua inayofuata.

Klabu za Stoke City na Swansea zinamtaka nyota wa Celtic ambaye ana ukongwe wa kipekee sana katika soka ili avipe hamasa vikosi vyao. Mkataba wa nyota huyo, Jonny Hayes na klabu hiyo upo mwishoni hivyo atakuwa anapatikana kwa usajili huru kwa klabu itakayohitaji huduma yake.

Acha ujumbe