Ikiwa ni Jumatatu murua kabisa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kufungia viwanja vitatu kutumika kwa michezo ya ligi kutokana na kukosa vigezo vya kikanuni na kisheria vinavyotakiwa kutumika kwa Ligi Kuu.
Taarifa hiyo imesema kuwa viwanja vilivyokumbana na rungu hilo ni Jamhuri (Dodoma), CCM Kirumba (Mwanza) na Liti (Singida).
Taarifa iliyotolewa leo Machi 10, 2025, na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo imesema miundombinu ya viwanja hivyo haikidhi masharti yaliyowekwa katika Kanuni ya Leseni za Klabu.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Hivyo, timu zinazotumia viwanja hivyo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia viwanja vingine vinavyokidhi vigezo hadi marekebisho yatakapofanywa na TFF kufanya ukaguzi upya.
TFF imezikumbusha klabu zote kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja ili kuhakikisha michezo inachezwa katika mazingira salama na yanayokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.