Thiago Alcantara Kutoka Bayern Kwenda Liverpool

Kwa mujibu wa chanzo cha habari za michezo cha Argentina, Liverpool wanatarajiwa kukubaliana na dili la kumsaini Thiago Alcantara kutokea Bayern Munich kwa €35m

Taarifa zingine kutoka Hispania zilikuwa zikimtaja staa huyu kuwa yupo mbioni kujiunga na klabu ya Liverpool. Huenda anaweza kusogeza mabadiliko ya aina fulani kwenye safu ya kati klabuni Liverpool.

Staa huyu ni moja kati ya mastaa waliomaliza Akademi ya soka ya Barcelona. Kwa ujumla safari yake ya soka la kulipwa ilianzia Barcelona, akiichezea timu ya vijana toka mwaka 2006 hadi mwaka 2008.

Mwaka 2008 hadi mwaka 2011 alikuwa akiichezea Barcelona B. Mwaka 2011 aliingia rasmi kikosi kikuu cha Barcelona ambacho alitumikia hadi mwaka 2013 alipokamilisha uhamisho kwenda Bayern Munich.

Thiago Alcantara Kutoka Bayern Kwenda Liverpool
Thiago Alcantara

Ni moja ya mastaa wanaotajwa kuwa vizuri kwenye nafasi zao. Thiago ameona goli mara 3 katika mechi zake 35, katika michuano yote msimu huu. Inaweza kuwa ni magoli machache lakini anaonekana kuwa makini sana.

Hata hivyo, Mkurugenzi mkuu wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge, alishaweka wazi awali kuwa staa huyu anataka kuondoka. Mkurugenzi alitaja kuwa jitihada za mazungumzo ziligonga mwamba na inaonekana alikuwa ana mpango wa kufanya kitu ingine.

Karl-Hein alibainisha kuwa awali hawakuwa wamefanya mazungumzo na Liverpool lakini kama staa huyu atahitaji kwenda Liverpool watahitaji kufanya nao mazungumzo. Bayern Munich hawapo tayari kumpoteza bure wakati mkataba wake ukiwa unafika tamati mwisho wa msimu huu.

 

43 Komentara

    Habar njema sana 👍

    Jibu

    Imekaa vizuri Sana anakwenda Tim sahihi

    Jibu

    Axante kwa kutujuza

    Jibu

    Good newz

    Jibu

    Thiago alcantara ataenda kuimalisha kikosi, cha Liverpool msimu ujao

    Jibu

    Ipo poa sana acha aende liverpool

    Jibu

    Mwacheni aende tu Maisha popote

    Jibu

    Ni Jambo zuri kujiunga na mabingwa wapya wa EPL

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Kiungo fundi kwa Liverpool ataenda kufanya vizuri japo umri unakwenda#meridianbettz

    Jibu

    Nadhani Liverpool watauza wachezaji wengi sana msimu ujao ndo mana wanajihami mapema.

    Jibu

    Welcome to the champions

    Jibu

    Kila raheri katika klabu mpya#meridianbett

    Jibu

    Kila kheri kwake

    Jibu

    Mchezaji yoyote Yule anatamani kwenda kwenye mafanikio kwahiyo karibu nyumbani kwa Machampion..

    Jibu

    Habari njema Sana

    Jibu

    Habari njema kikosi kinaongezeka Liverpool mambo yanaenda poa hapo

    Jibu

    Habari njema sana#meridianbettz

    Jibu

    Mchezaji anae jituma sana na amekuwa ni moja kati ya mastaa waliomaliza Akademi ya soka ya Barcelona. Kwa ujumla safari yake ya soka la kulipwa ilianzia Barcelona, akiichezea timu ya vijana #meridianbettz

    Jibu

    Imekaa powa sana bora aende liverpool

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Thiago alcantara ni moja ya mastaa wanao tajwa kua vizuri kwenye nafasi zao sizani kama Bayern Munich watakua tayari kumpoteza

    Jibu

    Safari njema

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Liverpool mambo yanaenda vizur hapo

    Jibu

    Thiago Alcantara nibonge lamchezaji anajua nivizuri kalibige baba Liverpool

    Jibu

    Thiago ni mmoja wa mastaa wanaotajwa kua vizuri katika nafasi zao

    Jibu

    Thiago alcantara fundi Kama Liverpool watafanikiwa itakua bonge La deal Liverpool watakua moto sehemu ya kiungo

    Jibu

    ipo poa sana acha aende Liverpool

    Jibu

    Kama kaamua kwenda aende tu Liverpool ni timu kubwa sana atajifunza vitu vingi tofauti

    Jibu

    Maoni:Habari njema hii

    Jibu

    Alcantara moja ya viungo bora duniani na anastahili kuwepo kwenye kikosi shindani cha Liverpool,nafkiri Liverpool waendelee na hili dili kwani itakua dili zuri vile vile kujiwinda kwani kuna baadhi ya wachezaji tegemeo wanaweza kuondoka kusajiliwa timu nyingine

    Jibu

    Ingependeza kama angerejea Klabu yake ya zamani Barcelona ambao wapepwaya kiungo na Ulinzi. Heri kwao Liverpool kuendelea kuimarisha kikosi chao#meridianbettz

    Jibu

    Bado nina mashaka kama kweli Liverpool atawafaa huyu

    Jibu

    Habar njem a

    Jibu

    Huyu alcantara namkubali sana.

    Jibu

    liver wameamua sasa Klopp now yuko serious

    Jibu

    Hao Liverpool#Sasa Sifa#Meridianbettz

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Nikiungo bora hivyo anastahili kwenda kucheza liverpool

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    mambo n moto

    Jibu

Acha ujumbe