Thiago Motta mchezaji wa zamani wa vilabu vya Barcelona,Inter milan,pamoja PSG anatarajia kua kocha mkuu wa klabu ya Bologna inayoshiriki ligi kuu ya nchini Italia maarrufu kama Serie A.

Hii imetokea baada ya klabu hiyo kumfuta kazi aliekua kocha wake mkuu Sinisa Mihajlovic amabae ameiongoza klabu hiyo kwa michezo mitano ya ligi hiyo bila kushinda mchezo wowote na kuambulia alama tatu katika michezo hiyo mitano jambo ambalo limewafanya mabosi wa klabu hiyo kumfukuza kocha huyo kufuatia mwanzo mbaya wa msimu aliokua nao.

Kocha huyu alichukua nafasi ya kocha Rossoblu januari 2019 aliendelea kukiongoza kikosi hicho licha ya kutambulika na ugonjwa leukemia julai 2019 kabla kufutwa kazi jumanne ya wiki hii.

thiago mottaKocha wa vijana wa klabu hiyo Luca Vigiani atachukua usukuni kuiongoza timu hiyo katika mchezo wa jumapili wa ligi kuu Italia dhidi ya Fiorentina kabla ya Thiago Motta kuchukua nafasi ya kuiongoza timu hiyo kama kocha mkuu.

Baada ya kutundika daruga Motta alichukua jukumu la kufundisha vijana chini ya miaka 19 wa klabu ya PSG mwaka 2018 kabla ya kufundisha timu za Spezia na Genoa zinazoshiriki ligi kuu nchini Italia na kuziwezesha kumaliza nafasi ya 16 kwa vipindi tofauti.

Kutokana na wasifu huo Thiago sio mgeni katika ligi kuu nchini Italia ana uwezo wa kufanya vizuri katika klabu ya Bologna.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa