Thiago Silva anadai alibanwa sana wakati alipokuwa Paris Saint-Germain na anamshukuru Frank Lampard kwa kumleta Chelsea mwaka jana.
Beki huyo wa kati wa Brazil alikuwa akiongea baada ya ushindi wa 1-0 wa Blues dhidi ya Manchester City katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumamosi huko Estadio do Dragao.
Silva alikua mchezaji mkongwe zaidi kuichezea Chelsea kwenye fainali kubwa ya Uropa, akimpita Claude Makelele, lakini mchezaji huyo wa miaka 36 alidumu dakika 39 tu kabla ya kuumia.
Kai Havertz alipachika bao pekee la mchezo huko Porto dakika tatu baada ya Silva kutoka uwanjani wakati Chelsea ilikuwa timu ya tatu ya Waingereza, baada ya Manchester United na Liverpool, kubeba kombe zaidi ya mara moja.
Ushindi huo ulikuwa mtamu haswa kwa Silva, ambaye alicheza fainali na PSG dhidi ya Bayern Munich Agosti iliyopita katika mchezo wake wa mwisho kwa klabu kabla ya kuondoka kama mchezaji huru.
Miamba hiyo ya Ufaransa ilipungukiwa katika misimu yote minane ya Silva huko Parc des Princes, lakini beki huyo mzoefu anahisi hakufanyiwa haki kwa kudondoshewa lawama baada ya kushindwa kubeba kombe.
“Huu ni wakati muhimu zaidi katika kazi yangu,” aliiambia RMC Sport. “Haiwezi kusahaulika. Sikufanikiwa na PSG lakini leo nina furaha. Natumai PSG itaifanya siku moja, pia.
“Kila wakati PSG iliondolewa, watu walijaribu kutafuta mkosaji na mara zote ilikuwa mimi. Hiyo ni aibu kwa sababu nilitoa kila kitu.
Silva aliwasili Chelsea muda mfupi baada ya PSG kupoteza kwa Bayern Agosti mwaka jana baada ya kushawishiwa kujiunga na kocha mkuu wa wakati huo Lampard.
MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Alimuonesha njia nzuri
Asante kwa taarifa