Thiago Silva Arejea Nyumbani Fluminese

Beki raia wa Brazil anayekipiga katika klabu ya Chelsea Thiago Silva amerejea rasmi katika klabu yake aliyoanzia maisha ya soka ya nchini kwao Brazil klabu ya Fluminese baada ya kumaliza mkataba na klabu ya Chelsea.

Thiago Silva mwezi uliomalizika alitangaza kua ataachana na klabu ya Chelsea mwishoni mwa msimu huu, Huku beki huyo akihusishwa na vilabu kadhaa barani ulaya, Uarabuni, na klabu ya Fluminese lakini mwishowe ameamua kurudi nyumbani.thiago silvaBeki huyo wa kimataifa wa Brazil amesaini kandarasi ya miaka miwili na klabu ya Fluminese ambapo mkataba wake utamalizika mwezi Juni 2026, Ni wazi safari ya beki huyo barani ulaya imefikia tamati na sasa amemua kurudi nyumbani.

Safari ya beki huyo imekua ya mafanikio makubwa barani ulaya kwani amefanya vizuri kwenye vilabu vya Ac Milan, PSG, na klabu ya Chelsea akifanikiwa kubeba mataji ya ligi nchini Italia na Ufaransa, Huku akitwaa taji la ulaya akiwa na klabu ya Chelsea mwaka 2021.thiago silvaBeki Thiago Silva anatajwa moja ya mabeki bora kuwahi kucheza mpira wa miguu kutokana na ubora mkubwa ambao amekua akionesha kila alipopita, Lakini pia namna ambayo ameweza kua kwenye ubora kwa kipindi kirefu kwani beki huyo mpaka sasa ana miaka 40 lakini alikua anacheza soka kwenye daraja la juu.

Acha ujumbe