Thiago Silva Kubaki Darajani?

Kwa hakika, umri ni namba tu. Thiago Silva ameendelea kuwa mwenye kiwango thabiti katika idara ya ulinzi, licha ya kuwa na miaka 37 kwa sasa.

Silva alijiunga na Chelsea kwa mkataba wa mwaka mmoja lakini, amekuwa ni mchezaji wa muhimu kwenye kikosi cha Thomas Tuchel toka msimu uliopita. Ameisaidia The Blues kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na ameendelea kuwa kiongozi shupavu mpaka sasa.

Inasemekana kuwa, Thiago Silva anataka kuendelea kucheza barani Ulaya kwa mwaka mmoja zaidi. Matakwa ya Silva yanapewa nguvu na kile anachokitaka Thomas Tuchel na uongozi wa Chelsea.

Maongezi ya kuongeza mkataba wa Silva yanatajwa kuanza siku za usoni na, huenda tukaendelea kumuona Silva ndani ya Stamford Bridge licha ya kuwa na umri mkubwa kuzidi wachezaji wote wa kikosi hicho kwa sasa.


WIKI NJEMA NA CRAZY TIME CASINO!

Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe