Beki wa klabu ya Chelsea Thiago Silva anatarajiwa kuukosa mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa ulaya hatua ya 16 baada ya kupata majeraha katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Tottenham wikiendi iliyomalizika.
Thiago Silva ambaye amepata majeraha ya goti katika mchezo dhidi ya Tottenham anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita kama ilivyoelezwa hapo awali, Hivo moja ya michezo muhimu ambayo ataikosa mchezaji huyo ni dhidi ya klabu ya Borussia Dortmund wiki ijayo.Beki huyo wa kimataifa wa Brazil amekua kwenye ubora mkubwa licha ya umri wake kua mkubwa lakini amekua mhimili mkubwa kwenye klabu ya Chelsea, Ni wazi kukosekana kwake katika muda huo anaacha pengo kubwa ndani ya klabu ya Chelsea.
Klabu ya Chelsea imekua ikiandamwa na majeruhi msimu huu haswa kwenye safu ya ulinzi kwani kabla ya Thiago Silva walishapata majeraha mabeki kadhaa wa timu hiyo kama Reece James, Ben Chilwell, Wesley Fofana, pamoja Kalidou Koulibaly ambao kwasasa wamerejea.Klabu ya Chelsea kwasasa itakua inawategemea mabeki wake wa katikati ambao wataziba pengo la Thiago Silva ambao ni Benoit Badiashile, Kalidou Koulibaly, Wes;ey Fofana, pamoja na Trevoh Chalobah mabeki hao ndio watakua kwenye makaratsi ya mifumo ya kocha Graham Potter.