Juni 8, 1990 kwenye dimba la San Sirro mjini Milan Italia, dunia ilishuhudia moja ya maajabu makubwa ya soka yakitokea. Hiyo ilikuwa siku ya ufunguzi wa Kombe la Dunia ambapo mabingwa watetezi, Argentina, walikutana na Cameroon.

Argentina wakiwa na mtu aliyeogopwa zaidi duniani wakati huo, Diego Maradona, walishangazwa kwa kufungwa 1-0.

Thomas N'Kono, Thomas N’Kono na Mkono wa Gianluigi Buffon, Meridianbet
Maradona

Zaidi ya mfungaji wa bao, Francois Omam Biyik na ari ya upambanaji ya timu nzima, ushindi huu pia ulichangiwa sana na mikono ya kipa wa Cameroon, Thomas N’kono.

Thomas N'Kono, Thomas N’Kono na Mkono wa Gianluigi Buffon, Meridianbet

Kipa huyo aliyekuwa akiidakia klabu ya Espanyol ya Hispania, alifanya kazi kubwa ya kuzuia michomo ya Maradona, Buruchhaga na hata Canigia.

Thomas N'Kono, Thomas N’Kono na Mkono wa Gianluigi Buffon, Meridianbet

Miongoni mwa watu walioushuhudia mchezo huo ni dogo mmoja wa miaka 12, ambaye alikuwa na ndoto ya kuja kuwa straika au kiungo mshambuliaji mkubwa duniani.

Lakini baada ya kuiona mikono ya Thomas Nkono ikifanya yasiyowezekana, dogo akamfuata baba yake na kumwambia amebadili mawazo ya kuwa straika au kiungo, na sasa anataka kuwa kipa.

Baba yake akamkubalia, akisema yeye mwenyewe ndiyo ana maamuzi ya juu ya hatima yake.Dogo ninayemzungumzia hapa sasa ni mtu mzima mwenye miaka 42 na umebaki mwezi mmoja afikishe miaka 43, naye ni Gianluigi Buffon.

Miaka 5 baada ya kubadili mawazo, yaani 1995, ndoto yake ya kuwa kipa ikatimia aliposaini mkataba wake wa kwanza kama mwanasoka wa kulipwa, katika nafasi ya mlinda lango.

Thomas N'Kono, Thomas N’Kono na Mkono wa Gianluigi Buffon, Meridianbet

Kwa heshima ya shujaa wake, Thomas Nkono, Buffon akampa mwanaye jina la Thomas, kama kumuenzi mtu aliyemtamanisha ukipa.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?

Thomas N'Kono, Thomas N’Kono na Mkono wa Gianluigi Buffon, Meridianbet

SOMA ZAIDI

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa