Thomas Partey Kusalia Arsenal

Kiungo wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ghana Thomas Partey taarifa zinaeleza ataendelea kuitumikia klabu hiyo kuelekea msimu ujao baada ya kuhusishwa kuondoka.

Kiungo Thomas Partey alikua anahusishwa na vilabu kadhaa kutoka nchini Saudia Arabia wiki kadhaa nyuma, Vilevile pia klabu ya Juventus ya nchini Italia ilikua inamfukuzia lakini kiungo inaelezwa ataendelea kusalia kwenye viunga vya Emirates.Thomas ParteyKlabu ya Arsenal imeamua kumbakiza kiungo huku ushawishi mkubwa ni wa kocha wa klabu hiyo Mikel Arteta ambaye ameamua kiungo huyo aendelee kusalia klabuni hapo kwa msimu mwingine licha ya vilabu kadhaa kutuma ofa.

Arsenal wamejitoa kwenye mbio za kumuwania kiungo Southampton Romeo Lavia na sababu kubwa ni kujihakikishia kumbakiza kiungo Thomas Partey ambapo kwasasa mbio imebaki kwa Liverpool ambao wamebaki wenyewe kwenye dili la Lavia.Thomas ParteyKiungo wa kimataifa wa Ghana alikua moja ya wachezaji muhimu kwa klabu ya Arsenal msimu uliomalizika na pale alipokosekana pengo lake lilionekana, Kutokana na ubora huo washika mitutu wameona bado wanamuhitaji kiungo huyo.

Acha ujumbe