Thomas Tuchel amefungiwa kucheza mchezo mmoja, baada ya kutofautiana na Antonio Conte baada ya Chelsea kutoka sare na Tottenham.

tuchel, Thomas Tuchel: Afungiwa Mechi Moja na Faini ya Paundi 35,000 kwa Utovu wa Nidhamu., Meridianbet

Mjerumani huyo pia ametozwa faini ya paundi 35,000 na Chama cha Soka (FA), kwa utovu wa nidhamu baada ya kukiuka Kanuni ya FA (E3), huku Conte akitozwa faini ya paundi 15,000 baada ya mameneja wote kukiri utovu wa nidhamu, katika mfululizo wa makabiliano kwenye mchezo wao uliomalizika kwa sare ya 2-2 Jumapili Stamford Bridge.

tuchel, Thomas Tuchel: Afungiwa Mechi Moja na Faini ya Paundi 35,000 kwa Utovu wa Nidhamu., Meridianbet

Adhabu ya Tuchel ya kufungiwa mechi moja imesitishwa kwa muda, ikisubiri sababu kamili zilizoandikwa za uamuzi huo ili kumruhusu meneja wa Chelsea kuchukua nafasi yake dimbani, kwenye mechi ya Jumapili (kesho) ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Leeds.

“Tume huru ya udhibiti leo imeamuru kwamba Thomas Tuchel atozwe faini ya pauni 35,000 na kupigwa marufuku kuhudhuria mechi moja, na Antonio Conte atozwe faini ya pauni 15,000 baada ya kukiuka kanuni ya FA ya E3.

“Adhabu hii inaweza kukatiwa rufaa, na kifungo cha Thomas Tuchel cha mechi moja imesitishwa kwa muda kusubiri sababu za maandishi za tume huru ya udhibiti kuhusu uamuzi wake utakaotolewa kwa wakati ujao.”taarifa ya FA.

Tuchel na Conte walihusika kwenye ugomvi kwa muda wote wa derby hiyo, huku mameneja wote wakizozana kabla ya kupewa kadi nyekundu wakati wa mchezo na kutolewa nje na mwamuzi Anthony Taylor.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa