Kocha wa klabu ya Chelsea Thomas Tuchel amejikuta ameingia kwenye kwenye vita na chama cha soka nchini Uingereza FA kutokana na kauli yake shutuma dhidi ya mwamuzi aliyechezesha mchezo wao siku ya jumamosi dhidi ya Tottenham.

Mchezo kati ya Chelsea na Tottenham ulikuwa ni wakuvutia na wenye hamasa kubwa kwenye dimba la Stamford Bridge ambao ulimalizika kwa timu hizo mahasimu kutoa sare ya goli 2-2 na kushuhudia makocha wao kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye dakika za mwishoni.

Thomas Tuchel, Thomas Tuchel Kauli Zake Zamuweka Matatani FA, Meridianbet

Kutokana na kauli alizotoa kocha wa klabu ya Chelsea Thomas Tuchel dhidi ya mwamuzi Anthony Taylor kwa kushindwa jumpa kasi nyekundu mlinzi wa klabu ya Tottenham kwa kumvuta nywele Cucurella.

Thomas Tuchel alipoulizwa kuhusu ikiwa ni bora kama Taylor asiwe mwamuzi wa michezo ya Chelsea tena, Tuchel alijibu: “Huenda itakuwa bora. Lakini kiukweli, Tulikuwa na VAR ya kutusaidia kufanya maamuzi  sahihi. Tang lini chezaji akavutwa nywle? Tangu lini hilo?  Na kama hakuona siwezi hilo, siwezi kumlaumu.

“Sikuona hilo, lakini kuna watu kwenye VAR ambao wanaangalia hili na kisha kukuonyesha na kwanini hii haiwezi kuwa  free-kick na kwanini hii haikuweze kuwa Kadi nyekundu? Inakuwaje?”

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa