Thomas Tuchel Kufanya Kazi na Watu Wake.

Kocha mpya wa Chelsea, Thomas Tuchel, anatarajia kuwaleta watu wake anaowaamini katika benchi lake la ufundi.

Tuchel amekabidhiwa mikoba ya Frank Lampard ambaye alioneshwa mlango wa kutokea Stamford Bridge baada ya kuiongoza timu hiyo kwa miezi 18. Kibarua cha kwanza kwa Tuchel kilikuwa ni mchezo dhidi ya Wolves ambapo walimaliza kwa sare ya 0-0.

Imeripotiwa kuwa, Thomas Tuchel anatarajia kumleta Arno Michels ambaye atakuwa ni msaidizi wake na Zsolt Low pia ataungana nae kwenye benchi lake la ufundi katika klabu ya Chelsea.

Thomas Tuche
Tuchel alipokuwa PSG.

Chelsea itatoatamko rasmi kuhusu uteuzi wa benchi jipya la ufundi ambapo, Michels amekuwa msaidizi wa Tuchel tangu alipokuwa Borussia Dortmund na hata PSG. Pia, Tuchel alivutiwa na uwezo wa Low alipokutana naye PSG na anatarajia kuendelea kufanya nae kazi katika EPL.

Imeripotiwa kuwa, Tuchel ni mtu anayependa kufanya kazi na watu anaowaamini. Hii ni sababu kubwa inayomfanya aambatane na benchi lake la ufundi kwenye kila timu aliyoifundisha mpaka sasa.

Licha ya Chelsea kumtimua Lampard, klabu hiyo imeadhimia kuwabakiza baadhi ya watu waliokuwa wakifanya nae kazi, hii ikiwa ni pamoja na Joe Edwards, Anthony Barry, Henrique Hilario, Matt Birnie na Will Tullett ambapo hawa wote walionekana wakisaidiana na Thomas Tuchel kwenye uwanja wa mazoezi kuelekea mchezo dhidi ya Wolves.


MSHINDANI HUSHINDA BWANA!

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!

Fairy-in-Wonderland_Casino-Post_25-January

CHEZA SASA

12 Komentara

    Vizuri

    Jibu

    Safi Sana kazi nzuri

    Jibu

    Kazi nzuri 👏👏

    Jibu

    Vzr

    Jibu

    Tunasubilia kuona chelsea ikiinuliwa na tuchel

    Jibu

    Safiiiii sana

    Jibu

    Inapendeza

    Jibu

    Vizuri

    Jibu

    Tuchel anamzigo mkubwa sana kubadilisha hali iliyopo sasahivi Darajani

    Jibu

    Tuchel imeingia kwenye kaa la moto

    Jibu

    Tuchel kazi anayo

    Jibu

    Shughuli ipo

    Jibu

Acha ujumbe