Thomas Tuchel Kuongezwa Miaka 3 Darajani.

Mcheza kwao hutunzwa! Thomas Tuchel yupo mbioni kupongezwa kwa kazi nzuri aliyoifanya tangu kukabidhiwa mikoba ya Frank Lampard pale Stamford Bridge.

Tuchel alipewa mkataba wa miezi 18 ukiwa na vipengele ambavyo vinategemea mafanikio ya ndani ya uwanja. Kati ya vipengele hivyo ilikuwa ni mafanikio ya Ligi ya Mabingwa na kuingia kwenye nafasi 4 za juu kunako EPL.

Kocha huyo amekuwa ni mkombozi kwa mashabiki wa The Blues na amerejesha furaha na matumaini makubwa kwa mashabiki wa timu hiyo kwa muda mfupi alioiongoza timu hiyo baada ya Lampard kuachishwa kazi pale darajani.

Chelsea ipo kwenye fainali 2 – Kombe la FA na Uefa huku ikiwa nafasi ya 4 kwenye msimamo wa EPL mpaka sasa. Imeripotiwa kuwa, uongozi wa klabu hiyo unatarajia kumuongezea mkataba Thomas Tuchel mwishoni mwa msimu huu.

Tuchel (kushoto) akizungumza jambo na Ng’olo Kante (kulia)

Kwa sasa, Thomas Tuchel anamkataba unaopatia takribani pauni milioni 7 na mkataba mpya wa miaka 3 utaongeza mapato yake maradufu. Japokuwa, kwa sasa lengo kubwa la Tuchel ni kumaliza msimu kwa mafanikio makubwa akizitazama fainali zote 2 kwa ukubwa wake sambamba na kujihakikishia nafasi 4 za juu kunako msimamo wa EPL.

Pamoja na Tuchel, Chelsea pia wanampango wa kumuongeza mkataba kiungo wao kisiki – Ng’olo Kante ambaye amekuwa ni muhimili mkubwa kwenye kikosi cha kocha huyo. Hakika Chelsea wanajambo lao kuelekea msimu ujao wa EPL.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

CHEZA HAPA

9 Komentara

  Dili nene hilo pongezi kwake

  Jibu

  Hongera sana Thomas

  Jibu

  Hongera sana

  Jibu

  Safi sana

  Jibu

  Good

  Jibu

  Hongera sana

  Jibu

  Safi sana azidi kukaza buti

  Jibu

  Tuchel piga kazi

  Jibu

  Vizuri

  Jibu

Acha ujumbe