Aliyekua mchezaji wa FC Bayern Munich na mchezaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Corentin Tolisso, ameachana rasmi na klabu ya Bayern Munich.
Baada ya kuwa pamoja kwa miaka 5, Tolisso na Bayern wameachana rasmi kwa kushindwa kuafikiana makubaliano ya mkataba mpya kati yao.
Haijajulikana wazi kikwazo katika mazungumzo ya mkataba mpya kilikua kitu gani lakini, sasa ni rasmi Corentin yupo sokoni kama mchezaji huru. Orodha ya wachezaji huru inaongezeka baada ya Marcelo, Isco na Bale kuingia kwenye kundi hili wakitokea Real Madrid.
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!