Tomiyasu Aongeza Mkataba Arsenal

Beki wa klabu ya Arsenal raia wa kimataifa wa Japan Takehiro Tomiyasu amefanikiwa kuongeza mkataba wa kuendelea kuwatumikia washika mitutu hao kutoka jiji la London.

Beki Tomiyasu ameongeza mkataba ambao utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2026 hii ina maana mchezaji ameongezewa mkataba wa miaka miwili tu, Kwnai mkataba wake ulikua unafika ukingoni mwishoni mwa msimu huu.tomiyasuBeki huyo ambaye alijiunga na klabu ya Arsenal akitokea klabu ya Bologna ya nchini Italia amekua akitumika kama beki wa pembeni ndani ya klabu hiyo, Nafasi ambayo amekua akiitendea haki kwa kiwango kikubwa.

Mjapan huyo inaelezwa ameongezewa mkataba wa miaka miwili tu kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara ndani ya timu hiyo, Kwani licha kuonesha ubora pale anapopewa nafasi lakini majeraha ni moja ya mambo yanayomkwamisha sana beki huyo.tomiyasuArsenal wameendelea kuwaongezea wachezaji wake muhimu mikataba na Takehiro Tomiyasu amekua miongoni mwa wachezaji hao, Kwani Arsenal wana mpango wa kutengeneza timu bora sana ambayo itafanya vizuri kwa muda mrefu kwenye ulimwengu wa soka.

Acha ujumbe