Toni Kroos Aitwa kwa Mara ya Kwanza Ujerumani

Kiungo wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Ujerumani Toni Kroos amefanikiwa kuitwa kwenye timu ya taifa ya Ujerumani kwa mara ya kwanza baada ya kutangaza kustaafu timu kuichezea timu hiyo.

Toni Kroos alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani punde tu baada ya kutolewa kwenye michuano ya Euro mwaka 2021, Lakini mwezi uliopita alitangaza kurejea kuitumikia timu hiyo.Toni KroosTaarifa zinaeleza kua chama cha soka cha Ujerumani kilifanya mazungumzo na kiungo huyo ili aweze kuitumikia timu hiyo kwenye michuano ya Euro mwaka huu itakayofanyika nchini humo na kiungo huyo alikubali ombi hilo na kutangaza kurejea tena kwenye timu hiyo.

Chama cha soka cha Ujerumani inaelezwa kiliona bado kiungo huyo ana nafasi ya kuendelea kutumikia kikosi cha wababe hao mabingwa mara nne wa dunia, Kiungo huyo wa Real Madrid anaonekana bado ana uwezo mkubwa kwani hata ndani ya klabu yake bado anaonesha ubora mkubwa sana licha ya kuwepo kwa vijana wadogo.Toni KroosSasa ni rasmi Toni Kroos atavaa uzi wa timu ya taifa ya Ujerumani kwa mara nyingine baada ya miaka mitatu kupita akiwa nje ya timu hiyo, Kiungo huyo ataitumikia Ujerumani kwenye michezo miwili ya kirafiki iliyo mbele yao wiki ijayo.

Acha ujumbe