Nyota wa Ujerumani Toni Kroos ameweka wazi wakati muhimu zaidi katika mchezo wa Real Madrid dhidi ya Bayern Munich.

Gwiji wa Ujerumani Toni Kroos, ambaye ni mmoja wa waliowahi kuwa nguzo ya Real Madrid, aliuchambua ushindi wa Bayern Munich wa mabao 2-1 dhidi ya Los Blancos katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Akizungumza kwenye podikasti yake, Kroos alisema: “Sikushangazwa na kilichotokea kwenye mchezo huo. Ingawa Bayern walicheza vizuri sana, kilichotokea baada ya kuwa wanaongoza 2-0 ndiyo kilikuwa cha kuvutia zaidi kutoka upande wa kisaikolojia.”
“Katika miaka ya hivi karibuni, Bayern wamekuwa wakiwadhibiti Real Madrid katika mchezo wa kwanza, lakini mara nyingi hushindwa kudumisha kiwango hicho au kufuzu kwenye mchezo wa marudiano mambo madogo madogo huishia kuwagharimu.”
Uongozi wa 2–0 wakati wa mapumziko ulipaswa kiakili kuufunga mchezo. Badala yake, Bayern Munich walirudi nyuma na kucheza kwa intensity ndogo zaidi katika ulinzi. Alisema Kroos.



