Torres Afichua Mawasiliano ya Arsenal Kabla ya Kombe la Dunia

Facundo Torres ambaye ni mshambuliaji amefichua kuwa Arsenal iliwasiliana na Orlando City kumtaka kabla ya Kombe la Dunia.

 

Torres Afichua Mawasiliano ya Arsenal Kabla ya Kombe la Dunia

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amevutia sana MLS tangu ajiunge nayo Januari 2022, akifunga mabao tisa na kutoa pasi nane za mabao katika mechi 33 katika msimu wake wa kwanza.

Torres ambaye ni mchezaji wa Kimataifa wa Uruguay amekuwa akipigiwa upatu kuhamia Ulaya tangu enzi zake akiwa na Penarol na Arsenal imekuwa ikihusishwa na kutaka huduma yake kwa muda mrefu.

The Gunners walimkosa Mykhaylo Mudryk kwa wapinzani wao wa London Chelsea, ambao waliingia kwa kasi na kuwashinda vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza katika kumsaka winga huyo wa Ukraine, lakini wamesalia sokoni kutafuta nyongeza za kuimarisha kikosi chao.

Torres Afichua Mawasiliano ya Arsenal Kabla ya Kombe la Dunia

Torres amefungua milango ya mbinu mpya, akielezea nia yake ya kucheza Ligi ya Primia.

“Orlando City ilinithibitishia kuwa kulikuwa na mawasiliano na Arsenal, lakini niliondoka kuelekea Kombe la Dunia na sikutaka kusikia kuhusu uwezekano wa uhamisho wakati huo,”.

Kwa hiyo mazungumzo yalibaki pale pale lakini sasa amerudi na timu wataona mazungumzo yanakwenda wapi, na angependa kucheza Ulaya kwani ni ndoto ambayo amekuwa nayo tangu akiwa mdogo kwasasa anaangazia Orlando City.

Torres Afichua Mawasiliano ya Arsenal Kabla ya Kombe la Dunia

Lakini La Liga au Ligi ya Primia wangekuwa walengwa wangu, na hapo ndipo uvumi unatoka. Lakini ndio, ningependa sana hilo. Alimaliza hivyo.

Acha ujumbe