Tottenham: Nuno Espirito Ahakikishiwa Kuwa na Kane

Kocha mpya wa Tottenham Hotspur Nuno Espirito Santo ameripotiwa kuhakikishiwa kuwa Harry Kane hataondoka klabuni hapo msimu huu wa joto.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anatamani kupata klabu mpya katika soko la sasa, na vilabu kadhaa, zikiwemo Manchester City na Manchester United, zinaendelea kutajwa kuwa na nia ya kupata huduma yake.

Tottenham: Nuno Espirito Ahakikishiwa Kuwa na Kane
Meneja mpya wa Tottenham, Nuno Espirito ahakikishiwa kuwa Harry Kane atasalia klabuni hapo

Kwa mujibu wa Daily Mail, meneja mpya wa Spurs Nuno ameambiwa kwamba klabu hiyo haina nia ya kumruhusu nahodha huyo wa England kuondoka kabla ya kampeni ya 2021-22.

Ripoti hiyo inadai kwamba Mreno huyo anajiandaa kuwa na Kane katika timu yake msimu ujao, na mwenyekiti wa timu hiyo Daniel Levy anakataa kupokea ofa.

Man City wanaaminika kuwa tayari kulipa ada ya pauni milioni 100 kwa fowadi huyo wa kati, lakini Levy anafikiriwa kumthamini mchezaji huyo nyota kwa zaidi ya pauni milioni 150.

Harry Kane Tottenham
Spurs walisema hawatopokea ofa yeyote yenye thamani ya chini ya pauni milioni 150 ili kumuachia Harry Kane anayehusishwa zaidi na Manchester City.

Kane ameifungia Spurs mabao 221 katika mechi 336 za mashindano yote, pamoja na mabao 33 katika safari 49 wakati wa kampeni za 2020-21, wakati pia akitoa asisti 17 katika muhula uliopita.

Msimu huu wa majira ya joto, mshambuliaji huyo ameifungia England mara moja katika mechi nne za Euro 2020.


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe