Klabu ya Tottenham Hotspurs imeendelea kuchechemea katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kufungwa tena leo katika mchezo wa ligi hiyo wakiwa nyumbani na klabu ya Newcastle United.tottenhamKlabu hiyo inapoteza mchezo wa pili mfululizo katika ligi hiyo baada ya kupoteza mchezo siku ya jumatano dhidi ya Man United katika dimba la Old Trafford na leo tena wakiwa nyumbani wamefungwa magoli mawili kwa moja na vijana wa Edie Howe.

Antonio Conte kocha wa Tottenham anaonekana kua kwenye wakati mgumu kwani klabu hiyo ilianza msimu vizuri lakini timu yake inaonekana kua kwenye wakati mgumu siku za karibuni baada ya kupoteza mchezo wao wa tatu kunako ligi kuu ya Uingereza msimu huu.tottenhamSpurs wameendelea kusalia katika nafasi ya tatu kwenye msimami wa ligi kuu ya Uingereza wakicheza michezo 12 huku wakiwa na alama 23 lakini wakiwa wamecheza mchezo mmoja zaidi ya klabu ya Chelsea na Man United ambao kama wakishinda michezo yao wataishusha klabu hiyo katika hiyo ya tatu.

Watu wengi wameonekana kutofurahishwa na mtindo wa uchezaji wa mwalimu Conte ambayo anaitumia ndani ya Tottenham ya kujilinda sana wakati huo ana wachezaji wengi wenye ubora wa kuweza kucheza soka safi na la kushambulia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa