Tottenham Kuachana na Lo Celso

Klabu ya Tottenham Hotspurs imepanga kuachana na kiungo wake raia wa kimataifa wa Argentina Giovani Lo Celso akiwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kwenye mkabata wake klabuni hapo.

Tottenham hawana mpango wa kuendelea na Lo Celso baada ya kuwepo klabuni hapo kwa muda kidogo akiwa hajawahi kutengeneza namba ya kudumu, Huku akiwa ni mchezaji wa ziada na kutolewa kwa mkopo mara kwa mara.tottenham

Vilabu kadhaa vimeonekana kuwinda saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Argentina kama klabu hiyo ya London Kaskazini itaachana nae, Huku moja ya vilabu hivo ni klabu ya Real Betis ya nchini Hispania ambao wanamuona kiungo huyo anawafaa klabuni kwao.

Mchezaji huyo nae ameonesha nia ya kutimka klabuni hapo huku mawakala wake wakiendelea kufanya mazungumzo na baadhi ya vilabu mbalimbali ambavyo vinataka saini yake, Huku wakiangalia ni klabu gani ambayo itakuja na ofa na nzuri ambayo mchezaji huyo atakubaliana nayo.tottenhamKlabu ya Tottenham wao wako kwenye mkakati wakuiboresha timu yao na kupunguza wachezaji ambao hawana matumizi nao ili kupisha wachezaji wengine watakaosajiliwa kwajili ya msimu ujao, Kwani klabu hiyo inaelezwa ina mkakati wa kuingia sokoni kwa nguvu kuiboresha timu hiyo kuelekea msimu ujao.

Acha ujumbe