Katika kujiandaa na usajili wa dirisha dogo mwezi Januari. Tottenham Hotspurs wanatajwa kumsajili beki kisiki wa Inter Milan – Milan Skriniar kwa dau la pauni milioni 45.

Inter Milan walithibitisha kuingia hasara kubwa kwenye mapato ya timu hiyo na inasemekana wanahitaji pesa kwa udi na uvumba. Kufuatia mtikisiko wa kiuchumi, Inter wapotayari kumuachia Skriniar endapo timu yeyote italipa dau la pauni milioni 45.

Kwa mujibu wa mwanahabari wa Italia – Fabrizio Romano ameripoti kuwa ” hali ya Milan Skriniar haijabadilika. Inter Milan wanahitaji pesa. Kama Spurs watafika kesho asubuhi na pauni milioni 45, Inter watamuuza [Skriniar].

“Usajili wa Skriniar upo mikononi mwa Tottenham kwa sasa.”

Jose Mourinho atakuwa amelamba dume kama Tottenham watamsajili Skriniar. Tayari Spurs wameshapoteza beki wako kisiki – Jan Vertonghen ambaye aliondoka kama mchezaji huru na amejiunga na Benfica.

Hali ni tete kuhusu hatma ya Toby Alderweireld na Davinson Sanchez ndani ya kikosi cha Spurs na tayari pengo la Vertonghen lilizibwa na usajili wa Joe Rodon akitokea Swansea. Kama Skriniar atatua Spurs, safu ya ulinzi katika timu hiyo itakuwa imeirika zaidi.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Tottenham, Tottenham Kumsajili Milan Skriniar., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

30 MAONI

  1. Hali ni tete kuhusu hatma ya Toby Alderweireld na Davinson Sanchez ndani ya kikosi cha Spurs na tayari pengo la Vertonghen lilizibwa na usajili wa Joe Rodon akitokea Swansea. Kama Skriniar atatua Spurs, safu ya ulinzi katika timu hiyo itakuwa imeirika zaidi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa