Klabu ya Tottenham Hotspurs imefikia uamuzi wa kumvunjia mkataba kiungo wake raia wa kimataifa wa Ufaransa Tanquy Ndombele kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Tottenham wanaachana na Ndombele baaada ya mchezaji huyo kutokua na ubora ambao wao kama klabu waliuhitaji au ambao waliouna wakati wakati wanamsajili klabuni hapo mwaka 2019, Sababu ya kuachana na kiungo ni kua hajakitimiza kile ambacho klabu hiyo ilikitarajia kutoka kwake.Tangu afike klabuni hapo mwaka 2019 Ndombele amekua ni mchezaji wa kutolewa kwa mkopo mara kwa mara na hii inakuja kutokana na mchezaji huyo kutokua na ubora, Ndombele amepita vilabu vya Olympique Lyon, Napoli, pamoja na Galatasaray.
Kuthibitisha kua mchezaji huyo hakua na ubora mkubwa ambao umewafanya Tottenham kuachana nae ni kua katika vilabu vitatu vyote alivyopita kwa mkopo hakuna klabu ambayo mwisho mkopo huo ilikaa mezani na Spurs kwajili ya kuhitaji huduma ya kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa uhamisho wa kudumu.Tanquy Ndombele atakua huru kuelekea msimu ujao hivo ni wazi kuanzia leo ataanza kufanya mazungumzo na vilabu ambavyo vitakua vinahitaji saini yake kuelekea msimu ujao, Huku vilabu hivo vikiwa vinapaswa kukubaliana na mchezaji huyo tu haswa kwenye eneo la maslahi kwani hawatatakiwa kulipa ada ya uhamisho kwakua mchezaji huyo ni huru.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.