Tottenham waanza na sare Epl

Klabu ya Tottenham Hotspurs imeanza na sare ya mabao mawili katika mchezo wao wa kwanza katika ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Brentford katika mchezo uliopigwa katika dimba la Gtech Community.

Klabu ya Tottenham walifanikiwa kupata bao la mapema tu kupitia kwa beki wake raia wa kimataifa wa Argentina Cristian Romero mano dakika ya 11 kabla ya Bryan Mbeumo kusawazisha dakika ya 26 ya mchezo.tottenhamMchezo uliendelea kua na kasi timu zote zikishambuliana kwa zamu kabla ya dakika ya 36 Yoane Wissa kuipatia Brentford bao la pili na la uongozi katika mchezo ambapo beki Emerson Royal kabla ya mapumziko na kupelekea mchezo kwenda mapumziko kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.

Mabao yote katika mchezo huo yalipatikana kipindi cha kwanza cha mchezo ambapo ulikua una mashambulizi ya hatari kwa kila timu, Lakini kipindi cha pili Spurs walionekana kutawala zaidi lakini hawakufanikiwa kuongeza bao.tottenhamKiungo James Maddison alikua kwenye ubora mkubwa kwani amehusika katika magoli yote yaliyofungwa na klabu yake ya Tottenham akiwa amepiga pasi zote za mabao katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu akiwa na klabu hiyo.

Acha ujumbe