Ingawa Randal Kolo Muani na Juventus wanaonekana kuwa na hamu ya kuungana tena, inaripotiwa kuwa Tottenham wanakataa kusitisha makubaliano ya mkopo na Paris Saint-Germain.

Mshambuliaji huyo tayari aliwahi kuichezea Juventus kwa mkopo kutoka PSG mwaka 2025, lakini klabu hizo zilishindwa kufikia makubaliano ya uhamisho wa kudumu.
Badala yake, alijiunga na Tottenham Hotspur kwa mkopo na alifunga jana usiku kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, jambo linalomfanya awe na mabao matatu na pasi tatu za mabao katika mechi 24 za mashindano yote akiwa na klabu ya Uingereza.
Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.
Kwa mujibu wa Sky Sport Italia, baada ya Kolo Muani kuonyesha nia ya kurejea Juventus, Tottenham walifunga kabisa milango.


