Tottenham Wamefikia Makubaliano na Empoli Kumnunua Golikipa Vicario

Tottenham Hotspur wanaripotiwa kukaribia kukubaliana rasmi juu ya dili la kumsajili golikipa Guglielmo Vicario kutoka Empoli.

 

Tottenham Wamefikia Makubaliano na Empoli Kumnunua Golikipa Vicario

Gianluca Di Marzio ameripoti kwamba makubaliano kimsingi yamefikiwa kati ya vilabu hivyo viwili, yakihusisha ada ya €20m pamoja na bonasi, huku Empoli ikitarajia ofa rasmi, iliyoandikwa kuwasilishwa ifikapo Alhamisi asubuhi.

Uhamisho wa €20m utafanya Vicario kuwa mauzo ghali zaidi katika historia ya klabu ya Empoli.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ametajwa kuwa mmoja wa makipa wa Italia waliofanya vyema zaidi katika kipindi cha 2022-23, akipangwa mara 32 kwa Empoli katika Serie A na Coppa Italia, akiruhusu 41 pekee kwa msimu huu.

Tottenham Wamefikia Makubaliano na Empoli Kumnunua Golikipa Vicario

Vicario alijiunga na Empoli miaka miwili iliyopita mnamo Julai 2021, awali akisaini kwa mkopo, kabla ya kufanya uhamisho wake kuwa wa kudumu msimu uliofuata.

Tangu wakati huo, mhitimu huyo wa akademi ya Udinese ameichezea klabu hiyo zaidi ya mechi 70 za kimashindano, na hatimaye kumaliza msimu huu katika nafasi ya 14.

Acha ujumbe