Tottenham Yakaa Kileleni Epl

Klabu ya Tottenham Hotspurs imefanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kushinda mchezo wao mchana huu kwa bao moja kwa bila dhidi ya Lutton Town.

Tottenham wanakaa kileleni wakitoka nafasi ya pili ambayo walikaa kuanzia wiki iliyomalizika, Ambapo kwasasa wanakaa kileleni kwa tofauti ya alama mbili wakiwa wana alama zao 20.TottenhamKlabu hiyo kutoka Kaskazini mwa jiji la London wamefanikiwa kupata ushindi licha ya kiungo wake Yves Bissouma kuonyeshwa kadi ya nyekundu dakika za nyongeza baada ya kujiangusha katika eneo la hatari kujaribu kumhadaa mwamuzi apate penati.

Goli la mchezo huo lilipatikana kipindi cha pili kupitia kwa Matty Van de Ven mapema tu dakika ya 52 ya mchezo, Bao ambalo lilifanikiwa kudumu kwa dakika zote za mchezo na kufanikisha Spurs kushinda mchezo.TottenhamKlabu ya Tottenham Hotspurs chini ya kocha Ange Postcoglou mpaka sasa wanaendeleza rekodi ya kutokupoteza mchezo wowote wa ligi kuu ya Uingereza na mpaka sasa wamefanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.