Klabu ya Tottenham Hotspurs ambao wameanza vizuri msimu wamekumbwa na wimbi la majeraha baada ya mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Chelsea.
Tottenham walipokea kichapo cha mabao manne kwa moja kutoka kwa majirani zao kutoka jiji la London klabu ya Chelsea, Lakini katika mchezo huo kulizalisha majeraha takribani wawili ambao ni beki Matty Van de Vien, Pedro Porro na kiungo James Maddison.Baada ya kupokea kipigo kutoka kwa klabu ya Chelsea na majereha nao wanakua kikwazo kuelekea michezo inayofata ya klabu hiyo, Kwani beki Van de Vien amekua moja ya wachezaji muhimu ndani ya timu hiyo kama ilivyo kwa James Maddison na Pedro Porro.
Licha ya majeraha ambayo waliyapata katika mchezo dhidi ya Chelsea majogoo hao kutoka jiji la London pia wana mchezaji Richarlison ambaye anatarajiwa kufanyiwa upasuaji, Vilevile beki Cristian Romero atakosekana katika michezo inayofata baada ya kuoneshwa kadi nyekundu.Klabu ya Tottenham Hotspurs ambayo inakamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza na imepoteza mchezo pekee mpaka sasa kwenye ligi hiyo majeraha ambayo wameyapata kwasasa yanaweza kua sehemu ya kuiyumbisha klabu hiyo kuelekea yao ya usoni.