Klabu ya Tottenham Hotspurs imekutana na kitu kizito baada ya kuambulia kipigo cha mabao manne kwa bila mbele ya klabu ya Newcastle katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.
Mchezo huo ambao umepigwa katika dimba la St James Park ulishuhudia klabu ya Newcastle United ikiisambaratisha Tottenham kwa kipigo kizito cha mabao manne kwa bila, Huku mbio za nafasi nne za juu zikiendelea kupamba moto.Newcastle walionekana kuuhitaji mchezo huo kwa kiwango kikubwa baada ya kufanikiwa kupata mabao mawili ya haraka dakika ya 30,32 kupitia kwa mshambuliaji Alexender Isak pamoja na winga Anthony Gordon na mchezo kwenda mapumziko Newcastle wakiwa mbele kwa mabao mawili.
Kipindi cha pili kilianza kwa Newcastle kuonekana kuendelea walipoishia kipindi cha kwanza, Kwani iliwachukua dakika sita tu ambapo dakika ya 51 Alexender Isak aliipatia tena Newcastle bao la tatu la mchezo huo.Klabu ya Tottenham ilionekana kufanya jitihada za kutaka kusawazisha bao lakini safu ya ulinzi ya Newcastle ilikua makini na kuhakikisha hawapati bao la kusawazisha, Huku wao wakipiga msumari wa mwisho dakika ya 87 kupitia kwa beki Fabian Schar na kufanikiwa kumaliza mchezo wakipata ushindi mnono.