Hali inaonekana sio shwari kwa beki wa kulia wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza Trent Alexander Arnold baada ya kuendelea kua kiwango kisichoridhisha hivi karibuni katika klabu hiyo yenye maskani yake jijini Liverpool.

Mchezaji huyo amekua akitupiwa lawama sana na baadhi ya wachambuzi na magwiji wa zamani wa mpira kutokana na aina ya uchezaji wake katika klabu hiyo na kudai ni mchezaji mzuri lakini amekua na makosa ya kujirudia mara kwa mara.

trent alexander arnoldTrent Alexander Arnold ambaye amekua kwenye kikosi cha Liverpool kilichofanya vizuri kwa takribani miaka minne sasa akipandishwa kutoka timu ya vijana ya klabu hiyo, Amekua akicheza kwa kiwango bora sana haswa katika upande wa kushambulia huku akionekana kua na kwango cha kawaida katika uzuiaji jambo ambalo linawafanya watu wengi kuamini beki huyo bado hajakamilika kama mchezaji wa kiwango cha dunia.

Lawama zimekua nyingi zaidi msimu huu ambao klabu yake inaonekana kuchechemea huku safu yao ya ulinzi ikiwa inaruhusu mabao kiurahisi zaidi huku huku upande wa mchezaji Trent Alexander Arnold ukionekana kama unapwaya zaidi na kusababisha manneno mengi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza.

trent alexander ArnoldKocha wa klabu hiyo Jurgen Klopp amekua akimtetea mchezaji wake huyo mara kwa mara lakini hali bado mchezaji huyo anaonekana kua na makosa mengi linapokuja suala la uzuiaji.Katika mchezo wa jana ambapo Liverpool walipata suluhu wakiwa nyumbani ya mabao matatu kwa matatu dhidi ya Brighton Hove Albion miongoni mwa magoli yaliyofungwa beki huyo alihusika na kuchochea hoja ya kua beki huyo hatoshi katika nafasi hiyo na anahitajika kupumzishwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa