Klabu ya Liverpool imetangaza kumuongeza mkataba beki wake Trent Alexander-Arnold katika tovuti ya klabu hiyo. Mkataba mpya utadumu hadi mwaka 2025.
Trent Alexander-Arnold ameichezea Liverpool jumla ya mechi 179 hadi sasa baada ya kutoka kwenye mfumo wa akademi ya klabu.
“Nimefurahi kupewa nafasi na kuonyeshwa uaminifu kwa klabu kuongezewa muda wa kuepo hapa” Alexander-Arnold aliiambia Liverpoolfc.com.
“Sehemu ambayo klabu ipo na mahali mimi nilipo katika taaluma yangu daima ni chaguo nzuri kwangu. Kukua na kuhakikisha kuwa niko hapa tena ni jambo zuri kila wakati. Nimetengenezwa hapa.
“Ni klabu pekee ambayo nimewahi kuijua, kwa hivyo kuwa hapa kwa muda huu na kuendelea kuwa hapa kwa muda mrefu ni jambo la kushangaza kwangu na familia yangu.
“Ni wakati wa kujivunia kwangu – siku zote – kusaini mkataba mpya hapa. Kupewa uaminifu, kama nilivyosema hapo awali, kwa klabu na wafanyakazi ni hisia ya kushangaza.”
SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!