Trent Ttarejea Dhidi ya Tottenham

Beki wa klabu ya Liverpool Trent Alexender Arnold amesema wanahitaji kurudisha matumaini katika mchezo wao ujao dhidi ya klabu ya Tottenham Hotspurs.

Klabu ya Liverpool wamepoteza mchezo jana dhifdi ya klabu ya Leeds United wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani, huku wakiwa na muenendo mbaya zaidi katika ligi hiyo msimu huu.trentKlabu ya Liverpool msimu huu imefanikiwa kushinda michezo minne tu katika michezo 12 waliyocheza katika ligi hiyo msimu. Huku ukiwa ni wastani wa chini katika misimu ya hivi karibuni kwa klabu hiyo.

Kutokana na hali hiyo beki wa kulia wa klabu hiyo Trent anaona mchezo unaofuata wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Tottenham wanatakiwa kupata ushindi ili kurejea kwenye hali ya ya kawaida.trent“Tunahitaji kwenda huko na kupata alama ikiwa tuna nafasi yeyote ya kufikia malengo na matarajio yetu msimu huu”Alisema Trent akilenga mchezo wao dhidi ya Spurs unaweza kua sehemu ya wao kurejea na kuweza kufikia malengo waliyojiwekea msimu huu kama klabu.

Acha ujumbe