Mchezaji wa Brighton Leandro Trossard amefunga hat- trick yake ya kwanza EPL kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya 3-3, ambapo mchezo huo ulikuwa wa kusisimua ambapo Liverpool ndio walikuwa wenyeji wa mchezo huo pale Anfield.

 

Trossard Apiga Hat-trick Yake ya Kwanza.

Mabao mawili ya kuongoza ya Trossard katika dakika ya 17 za mwanzo ziliipa timu hiyo kasi ya nguvu katika mchezo wa kwanza wa kocha mpya ambaye ni Roberto De Zerbi. Liverpool walipata bao kupitia kwa Roberto Firmino kabla ya mapumziko na mshambuliaji huyo wa Brazil akasawazisha mapema katika kipindi cha pili cha mchezo ambao ulikuwa wa kuvutia.

Sare hiyo ilimpa Zerbi nguvu ya kujitafuta na kuangalia wapi ataanzia, huku goli la tatu la Liverpool lilitokana na Brighton kujifunga.

Trossard Apiga Hat-trick Yake ya Kwanza.

Trossard anakuwa mchezaji wa tatu kwenye Ligi kuu ya Uingereza kufunga Hat-trick, baada ya mchezaji wa Manchester City Erling Haaland kufunga mara mbili na Son wa Spurs kupiga hat-trick mara moja. Hivyo mpaka sasa wachezaji waliopiga hat-trick ni wa tatu tuuh.

Brighton wamekuwa bora sana kadri siku zinavyozidi kwani mpaka sasa wapo nafasi ya 4 na wamepoteza mchezo mmoja tuu huku wakiendelea kuleta ushindani kwa wapinzani wao.

Trossard Apiga Hat-trick Yake ya Kwanza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa