Aliyekua Winga wa klabu ya Brighton Hove and Albion Leandro Trossard amefanikiwa kujiunga na vinara wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya soka ya Arsenal.
Klabu ya Arsenal imefanikiwa kukamilisha dili la winga Trossard kutoka klabu ya Brighton jioni ya leo kwa ada ya uhamisho ya € milioni 27, Na mchezaji huyo anatarajiwa kuelekea jijini London haraka ili kufanya vipimo vya afya na kusaini mkataba rasmi na kuanza kuitumikia klabu hiyo.
Dili la winga huyo limeenda haraka sana kutokana na hofu ambayo wamekua nayo klabu ya Arsenal kwani wamepokonywa tonge mdomoni na klabu ya Chelsea, Hivo walihitaji kukamilisha dili hili haraka iwezekavyo lisije likaingiliwa kama ambavyo Chelsea walifanya kwa mchezaji Mykhaylo Mudryk.
Winga huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anakwenda kuongeza nguvu ndani ya klabu ya Arsenal ili kuhakikisha wanaendeleza ubora wao msimu huu na kuendelea kukimbiza ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza ambao imeonekana klabu hiyo inauhitaji baada ya muda mrefu.
Taarifa kutoka klabu ya Brighton Hove and Albion inaelezw mchezaji Leandro Trossard ameondoka ndani ya timu hiyo kutokana na kutokua na maelewano mazuri na kocha wa klabu hiyo Roberto De Zerbi, Hivo kuondoka kwa mchezaji huyo ndani ya klabu hiyo lilikua jambo lisiloepukika.


