Mcheza Tenisi wa Ufaransa, Jo-Wilfried Tsonga ametangaza kustaafu kucheza tenisi ya kulipwa baada ya mashindano ya French Open kukamilika mwezi ujao.
Tsonga, 36, amekuwa na majeraha katika miaka ya hivi karibuni na aliambulia ushindi wake wa pili pekee tangu 2019 mnamo Februari, baada ya kukosa takriban msimu mzima wa 2020 na jeraha la mgongo na kuweka rekodi ya 1-8 mwaka jana.
“Kichwa changu kinaniambia, ‘unaweza kucheza maisha yako yote,’ na wakati huo huo mwili wako unakukumbusha kwamba uwezo wako wa haupo tena,” Tsonga alisema kwenye video iliyoweka kwenye mitandao yake ya kijamii.
Mcheza Tenisi huyo alimaliza wa pili katika michuano ya Australian Open mwaka wa 2008 na kufikia nusu fainali nyingine tano za Grand Slam.
Ameshinda mataji 18 ya ATP, ikiwa ni pamoja na mashindano mawili ya Masters 1000, tangu alipoanza kulipwa mwaka 2004. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 pia alishinda medali ya fedha ya Olimpiki katika mashindano mara mbili katika Michezo ya London mwaka wa 2012.
“Ninatumai kwamba nitaendelea kuwa katika hali nzuri na kuweza kuwa yule ambaye nimekuwa kwenye mashindano haya,” aliongeza Tsonga, akimzungumzia Roland Garros, ambayo itaanza Mei 22 hadi Juni 5.
“Lengo ni kuwa mimi, kuwa Jo-Wilfried Tsonga mchezaji wa tenisi…
“Siku zote nimejiwekea malengo ya juu kujaribu kupata kile ninachoweza. Kwangu, hii itakuwa nafasi ya kufanya hivyo kwa mara ya mwisho.” aliongeza Tsonga.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.