Taarifa rasmi kutoka Chelsea zinadai kuwa Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amefanikiwa kuongeza Mkataba wa miaka miwili na sasa atasalia klabuni hapo mpaka mwaka 2024.

Taarifa rasmi kutoka Chelsea ilisomeka kama ifuatavyo,

“Kocha wetu mkuu Tuchel alichukua mikoba rasmi mwezi Januari na kutusaidia kumaliza katika nafasi ya nne ya EPL, kitu kilichotuhakikishia kushiriki mashindano ya ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2021/2022 kabla ya kubeba kombe hilo msimu huu.”

Chelsea ikiwa chini ya Tuchel pia ilifanikiwa kufika fainali ya kombe la FA na goli moja tu la Leicester liliwafanya washindwe kubeba kombe hilo. Ila kombe kubwa zaidi lifika Stamford Bridge siku kadhaa zilizopita baada ya goli la Haverts kusalia mpaka mwisho wa mchezo.

Katika kuongeza mkataba wake, Tuchel alisema anafurahia sana kuongeza mkataba. Na anafurahia kuendelea kusalia hapo akiwa katika familia ya Chelsea.

TT pia aliahidi kuwa kuna mataji mengi zaidi anahitaji kupata akiwa na Chelsea na anaamini watafanikiwa wakicheza kwa pamoja kama timu.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa