Tuchel Asikitishwa Sare na Everton.

 

Meneja wa Chelsea, Thomas Tuchel ameonyeshwa kusikitishwa na matokeo ya sare ya 1-1 dhidi ya Everton katika mchezo wa jana wa Ligi kuu ya Premier nchini Uingereza.

 

Chelsea anashikilia nafasi ya tatu alama tatu nyuma ya Liverpool anayeshikilia nafasi ya pili na alama 4 nyuma ya mabingwa watetezi Manchester City wanaoshikilia nafasi ya kwanza katika msimamo.

“Inasikitisha kushindwa kupata ushindi katika mechi nyingine. Tunapoona jitihada tulizoingia nazo katika mechi kama hizi, jitihada za kufunga goli na mpinzani kusawazisha ni ngumu kuzipokea.” alisema Thomas Tuchel baada ya mchezo.

Tumepoteza nafasi kubwa kipindi cha kwanza na cha pili hatukuwa na muunganiko na tulijaribu kufanya mabadiliko, lakini ilikuwa ngumu. Tuliongoza na tukafungwa kwa mpira mmoja tu wa kutengwa.

“Ni kweli tumewakosa wachezaji wengi, wakubwa, wa kikosi cha kwanza, lakini isiwe sababu.” aliongeza Tuchel.


ANZA MSIMU WA SIKUKUU NA BURST THE BANK

Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe